Sunday, May 3, 2015

Pambano la Manny Pacquiao vs Floyd Mayweather

Je, uliuangalia mpambano kati ya Floyd Mayweather na Mannyy Pacquiao? Jambo moja lisilo shaka ni kwamba dunia imegawanyika kuhusu ni nani hasa alistahili ushindi! Wakati kuna wale wanaoamini Floyd Mayweather ameshinda kihalali kabisa, kuna wengine wengi tu wanaoamini kwamba ushindi ulistahili kwenda kwa Manny Pacquiao.

Majaji waliokuwa na wajibu wa kutenda haki walikuwa watatu. Miongoni mwa hao, jaji mmoja alimpa Floyd Mayweather ushindi wa points 118 dhidi ya 110 za Manny Pacquiao wakati majaji kila mmoja alimpa Floyd Mayweather points 116 dhidi ya 112 za Pacquiao.

Je, kwa maoni yako wewe, ni nani alistahili ushindi? Ikiwa hujaangalia pambano hili, basi gonga hapa uangalie mwanzo mpaka mwisho!
sss
Fuatilia pambano hilo kuanzia sekunde ya kwanza hadi ya mwisho.


Hiyo ndo hali halisi